Picha : DC SHINYANGA AWEKA JIWE LA MSINGI NA KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA BWALO LA CHAKULA SHULE YA LITTLE TREASURES



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Septemba 30,2017 ameweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School” iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.


Mbali ya kuweka jiwe la msingi pia ameendesha harambee kwa ajili ya kupata shilingi milioni 200 kwa ajili kukamilisha ujenzi huo,ambapo wazazi na walezi wameshiriki katika harambee hiyo. 

Akizungumza katika shule hiyo,Matiro aliwapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi kwa kujitoa kwa hali na mali kusaidia shule hiyo ambayo imejizolea sifa lukuki kwa utoaji wa elimu bora. 

“Shule hii imejizolea sifa nzuri,hii ni miongoni mwa shule bora kabisa nchini,kila mzazi anapenda mtoto wake asome kwenye shule nzuri,ukifika Shinyanga ukauliza shule gani nzuri,utatajiwa shule hii,nimeambiwa siri ya mafanikio haya inatokana na maono na utayari wa wazazi na marafiki kuisaidia shule hii”,alifafanua Matiro. 

“Sisi kama serikali tunaunga mkono sekta binafsi,kutokana na shule hii kufanya vizuri,ni ukweli usiopingika kuwa imeleta ushindani mkubwa kwa shule zetu za serikali,nasi kwa upande wa shule zetu za serikali hatuna budi kuiga, tuje kujifunza nini wanafanya hapa Little Treasures”,aliongeza Matiro. 

Aliwaasa wazazi na walezi mkoani Shinyanga kupeleka watoto shule kwani urithi pekee kwa watoto ni elimu na wala siyo mali ambazo hupotea kirahisi sana. 

Katika hatua nyingine alizitaka shule za taasisi binafsi kutoza ada zinazoendana na hali ya uchumi wa wazazi huku akiwasihi wazazi kutoa ushirikiano katika shule akitolea mfano wa shule ya Little Treasures ambayo imekuwa karibu zaidi na wazazi na walezi wa wanafunzi. 

Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic alisema ili kukamilika kwa jengo la bwalo la chakula jumla ya shilingi milioni 200 zinahitajika na tayari uongozi wa shule umetenga shilingi milioni 50 hivyo bado zinahitajika shilingi milioni 150. 

Naye Meneja wa shule hiyo,Wilfred Mwita alisema pindi jengo hilo litakapokamilika litatumika kama sehemu ya wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo kula chakula lakini pia kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo michezo na mikutano. 

Akisoma risala,Mkuu wa shule hiyo,Paul Kiondo alisema shule hiyo yenye mchepuo wa Kiingereza ina wanafunzi wa bweni na kutwa ilianza na wanafunzi wanne pekee na sasa ina jumla ya wanafunzi 662 kati yao,wavulana ni 304 na wasichana 318 na imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali.

Jumla ya shilingi milioni 15 zimepatikana katika harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula,ambapo wazazi na walezi pamoja na marafiki wa shule hiyo wamechangia huku Mkuu wa wilaya Shinyanga Josephine akitoa shilingi Milioni 2 pamoja na mifuko 30 ya saruji.


ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa pili kulia) akiwasili katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures “Little Treasures Nursery & Primary School”.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisoma maandishi baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures.
Maandishi yakisomeka kwa lugha ya Kiingereza yakiwa na maana ya 'Jiwe la Msingi limewekwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro leo Septemba 30,2017'.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya msingi Little Treasures.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimwagilia maji mti alioupanda katika shule ya Little Treasures.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiondoka katika eneo panapojengwa jengo la Bwalo la chakula katika shule ya msingi Little Treasures.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakimwongoza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika maaandamano kuelekea eneo la mkutano kwa ajili ya harambee kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika maandamano hayo.Wa kwanza kushoto mbele ni Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic,kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi.
Meza kuu: Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Kulia ni Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic,kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo,Tilulindwa Sulusi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika shule ya msingi Little Treasures ambapo aliipongeza shule kuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia wanafunzi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika shule ya msingi Little Treasures ambapo alisema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuinua kiwango cha elimu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwasisitiza wazazi kupeleka watoto shule kwani ndiyo urithi unaofaa kwa watoto.
Meneja wa shule ya Little Treasures Wilfred Mwita akizungumza wakati wa harambee hiyo ambapo aliwaomba wazazi na walezi wa wanafunzi pamoja na marafiki kuendelea kushirikiana na shule hiyo.
Mkurugenzi wa shule ya msingi Little Treasures,Lucy Dominic akizungumza wakati wa harambee hiyo ambapo aliishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana shule hiyo ili kuboresha kiwango cha elimu mkoani Shinyanga na nchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Little Treasures,Tilulindwa Sulusi akitoa neno.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akisoma risala.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza ngoma ya Kijaluo mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Wanafunzi wakicheza muziki.
Wazazi na walezi waliohudhuria mkutano huo wa harambee kuchangia ujenzi wa bwalo la chakula.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui naye alikuwepo katika harambee hiyo ambapo alichangia shilingi 500,000/- kusaidia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule hiyo.
Wazazi wakipiga makofi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza ngoma ya Kikurya.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba ngonjera.
Wazazi na walezi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Wazazi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
MC Mama Sabuni akifanya yake.
Wazazi wakiwa katika eneo la tukio.
Tunafuatilia kinachoendelea...
Walimu wa shule ya msingi Little Treasures wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri.
Wazazi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.
Waandishi wa habari wa magazeti ya Daily News na Habarileo,Suleiman Shagata na Kareny Masasy wakiwa katika eneo la tukio.
Waandishi wa habari John Mponeja wa Channel Ten na Getruda Mallya wa Radio Faraja wakifurahia jambo.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga,Said Pamui (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi Little Treasures Tilulindwa Sulusi wakiondoka katika shule hiyo baada mkutano wa harambee. 

Picha ya kumbukumbu mbele ya jengo la utawala shule ya msingi Little Treasures.

-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post