Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akizungumza katika mkutano wa jeshi la sungusungu 'Sanjo' wilaya ya Shinyanga leo Septemba 30,2017.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine amekutana na viongozi wa jeshi la jadi sungusungu kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo katika mkutano wa Jeshi la Sungusungu maarufu “Sanjo”.
Mkutano "Sanjo" umefanyika leo Jumamosi Septemba 30,2017 katika shule ya Msingi Ujamaa iliyopo katika kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili katika manispaa ya Shinyanga.
Sanjo hiyo imeandaliwa na jeshi la sungusungu halmashauri ya manispaa ya Shinyanga (Shinyanga mjini) na kuhudhuriwa pia na viongozi wa jeshi la sungusungu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Akizungumza katika ‘Sanjo’ hiyo,Matiro alilipongeza jeshi la jadi sungusungu kwa ushirikiano linaloutoa katika kukomesha vitendo vya kihalifu katika jamii na kwamba serikali inalitambua jeshi hilo na itaendelea kushirikiana nalo katika kuimarisha ulinzi na usalama katika jamii.
“Kwanza niwapongeze sana jeshi la sungusungu kwa kazi nzuri mnazofanya kwa kushirikiana na jeshi la polisi,bila unafiki,jeshi hili sisi kama serikali linatusaidia katika kuweka mambo sawa,wananchi wa Shinyanga wanaiogopa sungusungu kuliko polisi,huu ndiyo…ukitaka watu waende unavyotaka,wakabidhi sungusungu”,alisema Matiro.
“Tatizo la sungusungu kulalamika kusumbuliwa na polisi wakati wakifanya mambo yao hivi sasa halipo,tuliweka mambo sawa kwamba kesi za sungusungu zifuate mkondo wa sungusungu na suala hili sasa linatekelezeka,hakuna migongano tena”,aliongeza Matiro.
Aidha aliwataka kufuata sheria za nchi katika kutekeleza majukumu yao na kuacha kujichukulia sheria mkononi kama vile kuua watuhumiwa wa vitendo vya uhalifu na badala yake wawafikishe kwenye vituo vya polisi.
Naomba pia muwe wazalendo kwa nchi yenu,msiwafumbie mamcho wahalifufuateni sheria za nchi,ndiyo maana zile kanuni zenu niliomba ziende kwa mwanasheria ili mnapotekeleza majukumu yenu msibughuziwe”,alieleza Matiro.
Mkuu huyo wa wilaya aliliomba jeshi hilo kulinda amani ya nchi huku akiwasihi kuwa macho na baadhi ya watu wanaotaka kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Katika hatua nyingine aliwataka viongozi wa jeshi hilo kutumia faini na michango wanayochangiana kufanya masuala ya maendeleo ikiwemo kununua vyombo vya usafiri ili waweze kutekeleza majukumu yao vizuri badala ya kusubiri kuchangiwa.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa ya mkutano huo kuliomba jeshi la sungusungu kuhimiza wananchi kupanda miti ili kukabiliana na hali ya jangwa mkoani Shinyanga sambamba na kulima zao la pamba.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Sungusungu wilaya ya Shinyanga ya Shinyanga James Deshi alisema ushirikiano kati ya jeshi la sungusungu na polisi hivi sasa ni mzuri.
Alisema changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa ni usafiri wanahitaji pikipiki ili ziwasaidie katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Naye Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Claud Kanyorota aliyataja maeneo maeneo yanayoongoza kwa uhalifu katika wilaya ya Shinyanga kuwa ni Ngokolo na Bugweto na kwamba kwa kushirikiana na jeshi la sungusungu watakomesha vitendo hivyo.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akizungumza katika mkutano wa jeshi la sungusungu 'Sanjo' wilaya ya Shinyanga leo Jumamosi Septemba 30,2017 katika shule ya msingi Ujamaa kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akizungumza katika kikao hicho.Kulia ni Mwenyekiti wa jeshi la sungusungu wilaya ya Shinyanga Jiganza Jidula,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Claud Kanyorota akifuatiwa na diwani wa kata ya Mwamalili,Paul Machela.
Viongozi wa jeshi la sungusungu wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine akizungumza na viongozi wa jeshi la sungusungu.
Viongozi wa jeshi la sungusungu wakifurahia jambo katika mkutano huo.
Viongozi wa jeshi la sungusungu kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Shinyanga wakiwa katika mkutano huo.
Kamanda Mkuu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga,John Kadama akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa jeshi la sungusungu wilaya ya Shinyanga Jiganza Jidula akizungumza katika mkutano huo.
Viongozi wa jeshi la sungusungu Shinyanga mjini na Shinyanga vijijini wakiwa katika meza kuu.
Viongozi wa jeshi la sungusungu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
Katibu Mkuu wa Sungusungu wilaya ya Shinyanga James Deshi akizungumza katika Sanjo hiyo.
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza katika Sanjo hiyo.
Mkutano unaendelea.
Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Claud Kanyorota akizungumza katika sanjo hiyo.
Mkutano unaendelea.
Mkutano unaendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog