Picha : SHIRIKA LA KIVULINI LATOA MAFUNZO YA USAWA WA KIJINSIA,SERA NA SHERIA KWA WADAU SHINYANGA VIJIJINI

Afisa mradi wa “Usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana" kutoka Shirika la Kivulini lenye makao makuu yake jijini Mwanza, Eunice Mayengela akizungumza wakati wa mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia kwa wadau wanaotekeleza mradi huo leo katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akifungua mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia kwa wadau wanaotekeleza mradi wa “Usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana”. 
*****

Shirika la Kivulini limetoa mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia kwa wadau wanaotekeleza mradi wa “Usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana” kutoka kata ya Nyida,Nsalala na Itwangi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mradi huo unatekelezwa na Shirika la OXFAM kwa kushirikiana na shirika la Kivulini.

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo Alhamis Septemba 28,2017 katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga. 

Miongoni mwa wadau waliofaidika na mafunzo hayo ni maafisa maendeleo ya jamii,maafisa watendaji wa vijiji na kata,viongozi wa mabaraza ya kata,sungusungu,maafisa ustawi wa jamii,afya,wawakilishi kutoka dawati la jinsia wilaya ya Shinyanga.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo, Ofisa mradi kutoka Shirika la Kivulini lenye makao makuu yake jijini Mwanza, Eunice Mayengela alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa viongozi wa serikali za mitaa kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia.

“Tunatekeleza mradi wa “usawa wa kijinsia kiuchumi kwa wanawake na vijana katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Shinyanga Vijijini na leo tumekutana na wadau kutoka kata tatu za Nyida,Nsalala na Itwangi za Shinyanga Vijijini,lengo la mradi huu ni kujenga uwezo, uelewa na mikakati ya kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuzuia na kupambana na ukatili wa kijinsia”,aliongeza Mayengela.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,mgeni rasmi ambaye ni Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe alisema mafunzo hayo yatawasaidia wadau hao kutekeleza vyema majukumu yao katika kupinga na kupambana na ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao.

“Mafunzo haya yanajumuisha viongozi wa serikali za mitaa ambako ndiko matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yanafanyika,tumieni elimu hii kufikisha ujumbe kwa jamii kwamba ukatili wa kijinsia haukubaliki”,alisema Mgawe.

Alisema viongozi wa serikali za mitaa na maafisa ustawi wa jamii wana jukumu la kuwashauri waathirika wa vitendo vya kikatili juu ya haki zao kupeleka mashtaka ya ukatili katika vyombo vya usalama ikiwemo polisi na mahakama.

Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky alizitaja baadhi ya sababu za ukatili katika jamii kuwa ni wanawake wengi kuamini kuwa wao ni dhaifu,wanaohitaji kuongozwa,kuelekezwa na kuwajibishwa na wanaume pamoja na wanawake hao kukosa elimu kuhusu haki zao. 

Kwa upande wake,Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini,Deus Masili Muhoja aliwasihi viongozi wa serikali za mitaa kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na kuwasisitiza wawe tayari kutoa ushahidi ili waathirika wapate haki yao.

Afisa kutoka Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher aliwataka viongozi wa jeshi la jadi sungusungu kuimarisha usalama katika maeneo yao na wanapokamata mhalifu wamfikishe kituo cha polisi badala ya kujichukulia sheria mkononi kumwadhibu.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI UKUMBINI

Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akifungua mafunzo ya usawa wa kijinsia,sera na sheria zinazohusu usawa wa kijinsia akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini

Afisa Mradi kutoka shirika la Oxfam,Mkamiti Mgawe akizungumza ukumbini

Wadau wakifuatilia mafunzo
Afisa mradi wa kutoka Shirika la Kivulini,Eunice Mayengela akisisitiza jambo ukumbini.

Mafunzo yanaendelea....
Afisa mradi wa kutoka Shirika la Kivulini,Eunice Mayengela akizungumza ukumbini.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akitoa elimu kuhusu masuala ya ukatili katika jamii.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akielezea kuhusu ukatili wa kingono.

Bwana Beatu Berenardo kutoka kijiji cha Welezo kata ya Nsalala akichangia hoja ukumbini

Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini

Afisa Mtendaji wa kata ya Nyida Daudi Lazaro akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo,Glory Mlaky akiendelea kutoa mada wakati wa mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada ukumbini

Mwenyekiti wa Baraza la ardhi kutoka kata ya Itwangi,Joseph Maganga akichangia hoja ukumbini

Washiriki wa mafunzo wakifanya kazi ya kundi

Kazi za makundi zinaendelea

Kazi ya kundi inaendelea

Afisa Maendeleo wa kata ya Nsalala,Beatrice Macha akiwasilisha kazi ya kundi lake

Katibu wa jeshi la sungusungu kata ya Nsalala John Machiya akiwasilisha kazi ya kundi lake

Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini

Mwakilishi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher akizungumza ukumbini

Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini,Deus Masili Muhoja akizungumza ukumbini

Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo hayo.


Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post