Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka TCRA,Thadayo Ringo akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga leo.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa elimu kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kuhusu huduma ya watumiaji wa simu za mkononi kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu( Mobile Number Portability – MNP).
Elimu hiyo imetolewa leo Jumatano Septemba 27,2017 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga mjini Shinyanga.
Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka TCRA,Thadayo Ringo alisema elimu hiyo itawasaidia waandishi wa habari kupitia kalamu zao kuwaelimisha wananchi kuhusu huduma hiyo.
“Tumeamua kukutana na kundi muhimu la waandishi wa habari kwani kupitia vyombo vyenu vya habari mtaweza kufikisha elimu hii kwa watu wengi zaidi”,alieleza Thadayo.
Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kuwa makini wanapofanya miamala ya fedha kwenye simu zao ili kuepuka usumbufu unaojitokeza pale inapotokea wametuma pesa kwenda kwenye namba zisizokuwa sahihi.
“Nawasihi wananchi kuwa makini na matapeli wa mtandaoni,watu wengi wanatapeliwa mtandaoni kutokana tamaa ya kutaka faida haraka haraka,fanyeni kazi halali kwani mtu hawezi kuja kukutapeli kirahisi ofisini kwako,kumbuka kutapeli ni kosa la jinai,ukitapeliwa toa taarifa kituo cha polisi”,aliongeza Thadayo.
Naye Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano TCRA,Injinia Mwesigwa Felician alisema huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu inamsaidia mtumiaji wa simu kubaki na namba ya awali anapohama kutoka kwa mtoa huduma mmoja kwenda mwingine.
“Kupitia huduma hii utaweza kuchagua mtoa huduma anayekidhi mahitaji yako,unayeona anatoa huduma bora zaidi,huduma nzuri kwa wateja na mwenye ubunifu katika kutoa huduma zake”,alisema Felician.
Aidha alisema huduma hiyo inatolewa bure katika vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa na mtoa huduma unakotaka kuhamia.
Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari,mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde,aliishukuru TCRA kwa kutoa elimu hiyo na kwamba kupitia kalamu zao watafikisha elimu hiyo kwa wananchi.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka TCRA,Thadayo Ringo akitoa elimu kuhusu masuala ya mawasiliano kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.Picha zote na Suleiman Abeid na Kadama Malunde -Malunde1 blog
Naibu Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano kutoka TCRA,Thadayo Ringo akizungumza.
Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde1 blog akifuatilia mada ukumbini.
Mhandisi Mwandamizi wa Mawasiliano TCRA,Eng. Mwesigwa Felician akitoa elimu kuhusu huduma ya kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu( Mobile Number Portability – MNP).
Eng.Felician akiendelea kutoa elimu.
Waandishi wa habari wakifuatilia mada
Injinia Felician akiendelea kutoa elimu.
Mwandishi wa Radio Free Africa Malaki Philipo akiuliza swali ukumbini.
Kulia ni Mwandishi wa habari gazeti la Jamboleo Shaban Njia akiuliza swali kwa mwezeshaji.
Mwandishi wa habari na Mtangazaji kutoka Divine Fm ,Sumai Salum akisikiliza mada ukumbini.
Mwandishi wa habari na Mtangazaji kutoka Baloha Fm ,Michael Bundala akiuliza swali.
Kulia ni Mwandishi wa gazeti la Majira,Suleiman Abeid,kushoto kwake ni Afisa Habari mkoa wa Shinyanga,Magdalena Nkulu.
Kushoto ni Mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi pia Mweka Hazina wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Stella Ibengwe na Malaki Philipo wakifuatilia mada ukumbini
Mwandishi wa Clouds Media Zuhura Waziri na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Suzy Butondo wakiwa ukumbini
Kushoto (mbele) ni Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Kahama Fm,Neema Mghen na Mwandishi wa habari na Mtangazaji wa Radio Faraja Stephen Kanyefu,nyuma ni Kareny Masasy wa gazeti la Habari leo.
Kushoto ni Mwandishi wa habari gazeti la Majira,Patrick Mabula na Juma Mwesigwa kutoka HUHESO Foundation.
Mwandishi wa habari gazeti la Uhuru,Paul Kayanda akiwa ukumbini.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde akiandika dondoo muhimu.
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini. Wa kwanza kulia ni Afisa Habari mkoa wa Shinyanga,Magdalena Nkulu akifuatiwa na Sam Bahari wa gazeti la Mtanzania/Rai.
Kulia ni Mwandishi wa habari na Mtangazaji kutoka Divine Fm ,Sumai Salum,kushoto kwake ni Mwandishi wa habari gazeti Tanzania Daima,pia Katibu Msaidizi Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Ali Lityawi.
Mwandishi wa habari gazeti la Majira,Patrick Mabula akifuatilia mada ukumbini.
Mwandishi wa habari wa ITV/Radio One Frank Mshana akiuliza swali.
Kulia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe,Marco Maduhu akiandika dondoo muhimu.
Kushoto (mbele)ni Mwandishi wa habari na Mtangazaji kutoka Baloha Fm ,Michael Bundala na Neema Paul kutoka Divine fm.Aliyeko nyuma kushoto ni Pili Jitoba wa gazeti la Uhuru na Neema Sawaka gazeti la Nipashe.
Mwandishi wa habari gazeti la Jamboleo,Stephen Kidoyayi akisikiliza mada.
Waandishi wa habari na watangazaji kutoka Radio Faraja,Annastazia Paul (kushoto) na Jenifer Paul Mahesa (kulia).
Picha zote na Suleiman Abeid na Kadama Malunde -Malunde1 blog