Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2017 amemteua Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Uteuzi huu unaanza leo tarehe 10 Septemba, 2017.Kabla ya uteuzi huo Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amechukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ataapishwa kesho tarehe 11 Septemba, 2017 saa 4:00 Asubuhi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Septemba, 2017