Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Jumamosi amewatunuku Kamisheni maafisa 422 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamehitimu mafunzo mbalimbali kwenye chuo cha Jeshi Monduli mkoani Arusha.
Tukio hilo ambalo limefanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha Mjni, limehudhuriwa na viongozi mbali mabali wa kitaifa na mafisa wa Jeshi nchini pamoja na wananchi mbali mbali wa mkoa wa Arusha.
Kabla ya kuwatunuku kamisheni maafisa hao wa jeshi, Rais Magufuli alikagua gwaride maalum, na kutoa zawadi kwa maafisa wa jeshi watano waliofanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.
Tukio hilo la Rais Magufuli kuwapa Kamisheni Maafisa wa Jeshi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni la kwanza kufanyika katika uwanja wa wazi badala ya viwanja vya jeshi wilayani Monduli.
Social Plugin