Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kwa ushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani, na Ofisi ya rais TAMISEMI imesema itahikikisha Wanawake wanaojihusisha na biashara ya ukahaba wanaendelea kukamatwa ili kulinda hadhi ya mwanamke.
Hayo yamebainishwa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na watoto, Dkt. Hamis Kigwangala na kuwataka kuacha mara moja na kutafuta shughuli nyingine ya kujiingizia kipato.
Dkt. Kingwangala ametumia furasa hiyo pia kuwaasa wanaume ambao ndio wateja wakubwa wa biashara hiyo kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Katika hatua nyingine Dkt. Kingwangala amesema serikali imepiga hatua ya kupambana na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na hatua kadhaa wamezichukua ikiwemo kuzifungia baadhi ya taasisi zilizokuwa zinaashiria kuwasaidia watu wa aina hiyo.
Social Plugin