Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA FOUNDATION FOR TOMORROW LATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI SHULENI



Mkurugenzi wa shirika la Foundation for Tomorrow Melissa Queyquep akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Naura juzi jijini Arusha baada ya shirika hilo kudhamini shindano la kuwasaka wanafunzi bora katika masomo ya
Sayansi,Hesabu na Mawasiliano 
Meneja Mafunzo ya stadi za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrowa kulia akiwa katika picha ya pamoja mara baaada ya kumkabidhi mwanafunzi wa shule ya sekondari Arusha day zawadi ya fedha na cheti baada ya kuibuka mshindi katika shindano la kuwatafuta wanafunzi bora katika masomo ya Sayansi,Hesabu na Mawasiliano
Mkuu wa shule ya Sekondari Lemara Mkoani Arusha Risala  Juma akiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi wake wa kike kidato cha Nne shule ya Sekondari Lemara Victoria Kira aliyefanya vizuri katika somo la Sayansi
Afisa elimu Taaluma Sekondari jiji la Arusha Prosper Kessy wakati akizungumza kwa nyakati tofauti katika shule za Sekondari zilizopo katika jijili la Arusha zilizoshiriki
katika shindano la kuwasaka wanafunzi bora katika masomo ya Sayansi,Hesabu na Mawasiliano lililokuwa likiendeshwa na shirika la Foundation for Tomorrow
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Arusha day wakiwa wanafautilia kwa ukaribu

Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Naura
katika ni mwanafunzi aliyefa vizuri shuleni hapo akiwa na zawadi kulia ni  Meneja Mafunzo ya stadi
za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrow
Kulia ni Makamu Mkuu wa shule ya Arusha Day Dionisia Mrosso akiwa anapokea cheti kutoka kwa Meneja Mafunzo ya stadi za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrow
Na Pamela Mollel,Arusha
****
Wanafunzi hapa nchini wametakiwa kusoma kwa bidii wawapo mashule ili waweze kutimiza ndoto zao za baade huku wakishauriwa kutojiingiza katika makundi mabaya. 

Rai hiyo imetolewa juzi na Afisa elimu Taaluma Sekondari jiji la Arusha Prosper Kessy wakati akizungumza kwa nyakati tofauti katika shule za Sekondari zilizopo katika jijili la Arusha zilizoshiriki katika shindano la kuwasaka wanafunzi
bora katika masomo ya Sayansi,Hesabu na Mawasiliano lililokuwa likiendeshwa na shirika la Foundation for Tomorrow.

Kessy alisema kuwa lengo la wanafunzi hao kuwepo shuleni ni kusoma kwa bidii hali itakayowapelekea kufaulu vizuri masomo yao na ufaulu huo ni faraja kubwa kwa Serikali,wazazi pamoja na jamii

Kwa upande wake Meneja Mafunzo ya stadi za Maisha Hilda Lema kutoka shirika la Foundation for Tomorrow ambao ndio waaandaaji wa mashindano hayo alisema kuwa shindano hilo lilishirikisha shule 26 za Sekondari jiji la Arusha. 

Alisema lengo la shindano hilo ni kuwapa hamasa wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi,Hesabu na Weledi katika Mawasiliano (Insha) sanjari na kusaidia walimu
kugundua pengo katika masomo hayo na kuongeza bidii

Aliongeza kuwa katika shindano hilo walifanikiwa
kuwapata washindi  watatu hesabu,washindi watatu Sayansi,washindi wawili Insha ya Kiingereza na wawili Insha ya Kiswahili hivyo jumla ya washindi kumi walijinyakulia zawadi za fedha.

Alisema washindi wanne walipata shilingi 100,000,wanne 75,000 nawawili 50,000 na walimu wawili ambao walikuwa wakiwasaidia wanafunzi walioshinda katika masomo hayo waliweza kujinyakulia shilingi laki moja kila mmoja 

Kwa Upande wake mwanafunzi wa kike kidato cha Nne shule ya Sekondari Lemara Victoria Kira aliyefanya vizuri katika somo la Sayansi na kushika nafasi ya kwanza katika shindano
hilo alisema siri ya ufaulu wake ni kusoma kwa bidii.

Kira alitoa pongezi kwa shirika hilo kwa kuja na
wazo la kuwashindanisha wanafunzi katika masomo hayo ambapo shindano hilo linawapa hamasa wanafunzi na walimu shuleni.

“ Ndoto yangu kubwa nikuja kuwa Daktari bigwa hivyo
nawashauri wanafunzi wenzangu kutokukata
tama katika masomo yao bali waongeze bidii”,alisema Kira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com