Muda mfupi baada ya kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga kutangaza kutoshiriki katika marudio ya Uchaguzi Mkuu mpaka Tume ya Uchaguzi ifanyiwe mabadiliko, Tume hiyo imetangaza kundi la watu sita ambalo litasimamia uchaguzi huo.
Walioteuliwa ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Ezra Chiloba, Naibu wake Betty Nyabuto, Mkurugenzi wa Usajili wa wapiga kura pamoja na Mkuu wa Operesheni za Uchaguzi Immaculate Kasait, Naibu wake Mwaura Kamwati, Mkuu wa Operesheni za Tume na Mkuu wa Teknolojia James Muhati.
Uchaguzi wa marudio Kenya umepangwa kufanyika October 17, 2017 kutokana na ruhusa ya Mahakama ya Juu nchini humo kufuatia kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na Odinga.