Tundu Lissu akipandishwa kwenye ndege
***
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa CHADEMA na rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesafirishwa kwenda Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya matibabu usiku wa kuamkia Ijumaa Septemba 8,2017 baada ya kupigwa risasi akiwa Dodoma nchini Tanzania.
Ndege ya 5H-ETG iliyombeba Tundu Lissu imetoka katika uwanja wa ndege Dodoma saa sita na robo kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Agha Khan jijini Nairobi nchini Kenya.
Mbunge wa Rombo,Joseph Selasini amesema katika safari hiyo Tundu Lissu ameambatana na mkewe,madaktari wawili wasiokuwa na mipaka,mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mchungaji Peter Msigwa.
Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana siku ya Alhamis Septemba 7,2017 akiwa kwenye gari lake nyumbani kwake Dodoma.
Social Plugin