Baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kulieleza Bunge leo September 14, 2017 kwamba Mbunge wa Mpendae Salim Hassan Turky(CCM) alijitolea kuagiza ndege ya kumsafirisha Mbunge Tundu Lissu kwa ajili ya kumpeleka Nairobi, Kenya kwenye matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Dodoma ambapo baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wamepinga taarifa Spika.
Mbunge huyo amesema tukio la Tundu Lissu limemsikitisha sana na kuamua kukaa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali ambapo viongozi wa CHADEMA walitaka waende Nairobi lakini ndege haikuwa na kibali Kenya.
"Kutokana na uwezo niliojaliwa na Mungu nikatafuta ndege,ni ya rafiki yangu naruka naye sana,Chadema wakatafuta nauli zao dola 900 ili ndege iruke,ile ndege mimi ndiyo niliita, kwa kukubaliana na Mbowe wao ndiyo wamelipa",amesema Turky.
Social Plugin