Wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza hamu ya kufanya tendo la ngono katika ndoa kulingana na utafiti wa tabia za ngono uliofanywa nchini Uingereza.
Utafiti huo umebaini kwamba huku wanawake na wanaume wakionekana kupoteza hamu ya tendo la ngono kutokana na umri wao, wanawake wengi hupoteza hamu hiyo wanapoishi na wapenzi wao kwa muda mrefu.
Kwa jumla hali mbaya ya afya mbali na ukosefu wa uhusiano wa kihisia unaathiri hamu ya jinsia zote mbili ya kufanya tendo la ngono.
Matokeo hayo yanatokana na mahojiano ya wanaume 5000 na wanawake 6,700 yaliochapishwa na shirika la BMJ Open.
Watafiti hao wa Uingereza wamesema kuwa matatizo ya hamu ya ngono yanafaa kutibiwa kwa kumchunguza mtu badala ya kutumia dawa.
Mtaalam wa maswala ya ngono Ammanda Major amesema kuwa kwa binadamu kukosa hamu ya tendo la ngono sio swala lilisilokuwa la kawaida na kuna sababu nyingi tofauti ambazo wanaume na wanawake wanahitaji mabadiliko.
''Kwa wengine ni kawaida lakini wengine husababisha machungu mengi'' ,alisema.
Kwa jumla asilimia 15 ya wanaume na asilimia 34 ya wanawake waliofanyiwa utafiti huo walisema kuwa walipoteza hamu ya tendo la ngono kwa muda wa miezi mitatu ama hata zaidi katika mwaka uliopita.
Kwa wanaume, ukosefu huo wa hamu ya ngono ulikuwa juu miongoni mwa wanaume wa kati ya umri wa miaka 35-44 huku kwa wanawake ukionekana kati ya umri wa miaka 55 na 64.
Chanzo-BBC
Social Plugin