Mwanamme mmoja aliyetambulika kwa jina la Ashok Bharti nchini India ameuawa kikatili na Tembo baada ya kujaribu kupiga nae ‘Selfie’ .
Bwana Ashok Bharti (50), ambaye ripoti zinasema alikuwa amelewa na alimsogelea mnyama huyo kwenye mbuga ya Kuanrmunda iliyopo jimbo la Odisha state Kaskazini mwa India.
Kupitia video iliyorekodiwa na mashuhuda wa tukio hilo inaonesha Bwana Bharti akihangaika kukimbia baada ya Tembo aliyemkaribia kupiga nae picha kuanza kumkimbiza, lakini kwa bahati mbaya mbio hizo hazikufua dafu kwani alianguka na kukanyagwa na Tembo huyo aliyeonekana kukerwa na kitendo hicho.
Uongozi wa mbuga hiyo ulimchukua Bwana Bharti kwa Ambulance kumpeleka hospitali lakini kwa bahati mbaya alifia njiani.
“Ni kweli tukio limetokea Jumamosi ya tarehe 2 Septemba mwaka huu ambapo wanaume wanne walikuja kutembelea kwenye misitu yetu ambayo tumefuga tembo kwa ajili ya watalii lakini baadae tukasikia makelele ya watu hao ndipo tukaenda kuangalia tukakuta mmoja wao amejeruhiwa na Tembo tukampeleka Hospitali lakini kwa bahati mbaya alifariki njiani“,amesema Philip Sahu msimamizi wa Mbuga hiyo kwenye mahojiano yake na gazeti la India Times .
Kuanzia mwezi July mwaka huu mpaka Septemba tayari watu watatu wameuawa na Tembo kwenye vijiji vinavyozunguuka mbuga ya Rourkela, Tazama video ya tukio hilo.
Social Plugin