WABUNGE WA CHADEMA LEMA NA NASSARI WAKUBALI KUPELEKA USHAHIDI WA RUSHWA TAKUKURU

Wabunge wa Chadema, Godbless Lema na Joshua Nassari wamesema watapeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ushahidi kuhusu madiwani saba waliojiuzulu katika majimbo yao wanaowatuhumu kupokea rushwa ili kujiuzulu nafasi zao.


Lema ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini, amesema leo Jumatano kuwa, wanashukuru Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kuwakaribisha kupeleka ushahidi.


"Tunashukuru sana mkurugenzi mkuu wa Takukuru kutukaribisha, tutapeleka ushahidi wetu ofisini kwake na tunaamini atafanyia kazi tuhuma hizi," amesema.


Amesema mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki, Nassari ambaye madiwani watano katika jimbo lake wamejiuzulu amekwenda Nairobi nchini Kenya kuonana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kupata baraka zake kabla ya kwenda Takukuru.


"Nassari amekwenda Nairobi kuonana na Mwenyekiti Mbowe ili kumweleza tukio hili na akirudi tutakwenda naye moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Mlowola," amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post