Watoto watatu waliokuwa wakichunga ng'ombe katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli mkoani Arusha wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu walilolichezea wakidhani ni mpira.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Ijumaa jioni ambapo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Julius Mhale amesema watoto hao wanatarajiwa kuzikwa Jumatatu Septemba 18
Mwenyekiti huyo amesema kuwa eneo ambalo bomu lililipuka hutumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa mazoezi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa rasmi hapo baadae.
Social Plugin