Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.
Lukuvi amesema shamba lingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa.
Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.
Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa watashitakiwa.
"Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja," amesema.
Social Plugin