Mhasibu wa Shule ya Sekondari St Joseph, Elizabeth Asenga ametiwa hatiani kwa kosa la kumuita Rais John Magufuli kilaza.
Elizabeth ametiwa hatiani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa jamhuri kuthibitisha kosa.
Mhasibu huyo anadaiwa kuandika “hakuna rais kilaza kama yeye duaniani” katika mtandao wa kijamii wa Whatsapp.
Hakimu Shaidi akitoa uamuzi wa mahakama, alimtaka mshtakiwa huyo kulipa faini ya Sh milioni tano au jela mwaka mmoja ambapo amelipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Social Plugin