Mtu mmoja ambaye alikuwa mgonjwa kupitia kiasi amepoteza kesi yake katika mahakama ya juu kuhusu kusaidiwa kufa.
Noel Conway 67 , kutoka Shresbury nchini Uingereza ambaye anaugua ugonjwa wa neva alimtaka daktari kumpatia dawa itakayomuua wakati hali yake itakapozorota.
Kwa sasa daktari yeyote atakayemsaidia kufa atakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela.
Mawakili wake wanahoji kwamba amekwama katika chaguo lake ambalo halikumpendelea na kwamba sheria ilihitaji kubadilika.
Wanasema kuwa anaweza kujiua mwenyewe akiwa na uwezo wa kufanya hivyo ama asubiri kifo chake akiwa hana udhibiti kuhusu ni lini kitamkumba.
Awali amenukuliwa akisema kuwa ametaka kusema kwaheri kwa wapendwa wake katika wakati ufaao, sio kuwa katika hali ambayO hawezi kujielewa.
Amehoji kwamba wakati alipokuwa na chini ya miezi sita kuishi na kuwa na uwezo wa kutoa uamuzi , alitamani kupata usaidizi kutoka kwa daktari ili kuondoka duniani katika njia ya amani na yenye heshima kubwa.
Bwana Conway ambaye hakuwepo katika mahakama ya juu ya London siku ya Alhamisi alitaka uamuzi ambao sheria ya kujiua ya 1961 inaweka sheria ya kusaidiwa kufa, lakini haikubaliani na kifungu cha nane cha sheria ya Ulaya kuhusu haki za kibinaadamu.
Hii inatoa heshima kwa maisha ya kibinafsi na yale ya kifamilia na kifungu cha 14 ambacho kinalinda dhidi ya ubaguzi.
Lakini Jaji Sales na bi Whipple na jaji Garnham walikataa ombi lake.Bwana Conway akiteleza barafuni
Kabla ya kuugua bwana Conway alikuwa akipendelea mchezo wa kuteleza barafuni.
Chanzo-BBC