Keki Maalumu iliyoandaliwa na Azania Bank tawi la Moshi kwa ajili ya Wateja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakikata keki kwa pamoja kwa ajili ya kushiriki na Wateja wao ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea.
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakiwa katika muonekano tofauti ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.
Mfanyakazi wa Azania Bank ,tawi la Moshi ,Aida Mbilinyi akimuelekeza jambo mteja wa Benki hiyo Ibrahim Shoo alipofika katika tawi hilo kwa ajili ya kupata huduma.
Mfanyakazi wa Azania Bank,tawi la Moshi,Asifiwe Musa akiwa ni mwenye tabasamu wakati akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wa Benki hiyo waliofika kupata huduma.
Mfanyakazi wa Azania Bank,tawi la Moshi,Diana Ngaiza akimhudumia mmoja wa wateja wa Benki hiyo waliofika kwa ajili ya kupatiwa Huduma za kibenki.
Baadhi ya Wateja wakipata Huduma katika madirisha ya Huduma ndani ya Benki hiyo.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi ,Bi Hajira Mmambe akiwalisha keki baadhi ya Wateja waliofika kupata huduma katika Benki hiyo.
Wafanyakazi wa Azania Bank tawi la Moshi wakiwa katika picha ya pamoja nje ya jingo la Benki hiyo
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
Social Plugin