Mvua zinazoendelea kunyesha kuanzia jana mchana zimeanza kuleta madhara baada ya daraja la Kiluvya linalounganisha mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kukatika.
Kutokana na daraja hilo kukatika hudumza za usafiri wa magari ya abiria, mizigo na binafsi umesitishwa na wananchi wameombwa kutumia barabara ya Bagamoyo.
Daraja hilo ni kiungo muhimu kati ya jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa mbalimbali ya Kaskazini, Kati, Kanda ya Ziwa, Nyanda za juu Magharibu.
Aidha, mvua hizo zimesababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam yamejaa maji zikiwamo nyumba na kusababisha uharibifu wa mali.
Adha daraja lingine eneo la Mbezi beach jijini Dar es Salaam ‘maarufu la Jeshi’ kutokea Kawe limejaa maji na inadaiwa magari kadhaa yamezama na njia imefungwa.
Social Plugin