Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HIACE YAUA WATU WATANO BAADA YA KUGONGANA NA LORI MULEBA MKOANI KAGERA

Watu watano wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace kugongana na lori kisha kuwaka moto katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani Muleba mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Oktoba 20, saa 12:00 asubuhi.

Amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.

Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliopoteza maisha, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu.

Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com