JESHI LA POLISI SASA KUKOMAA NA MAADMIN WA MAGROUP YA WHATSAPP

Naibu mkuu wa kitengo cha makosa ya mtandaoni, Joshua Mwangasa amewataka viongozi wa makundi ya whatsApp kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika katika makundi yao kwani kwa kiasi kikubwa makundi hayo yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.


Ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa kutapunguza na kudhibiti makosa mengi yanayofanywa mtandaoni na kutasaidia polisi kuchukua hatua dhidi ya muhusika aliyefanya uhalifu huo.


Lengo kubwa likiwi ni kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu mtandaoni huku makundi ya What’s App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.


“Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata wewe utahusika,” amesema Mwangasa.


Mwangasa ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwahubiria waumini wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na uhalifu.


“Ukosefu wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi kwenu viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa maendeleo,” amesema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mamlaka hiyo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano mtandaoni.


Hayo yamezungumwa jana katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) na kuwakutanisha viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post