Kikosi Kazi kinachojumuisha Sekta kuu za matumizi ya Ardhi na Asasi za Kiraia wamekutana kwa ajili kuendelea kurejea
Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi, pamoja na kupongeza kazi nzuri ambayo inafanywa na kikosi kazi, lakini pia lizungumzia swala la mipango miji,upangaji wa mipango bora ya matumizi ya ardhi utakaozingatia mtazamo wa kuipeleka nchi katika Dira ya viwanda na pamoja na swala la mabadiliko ya Tabianchi, ili wananchi wawe tayari kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabianchi kunatakiwa kuwe na mipango mizuri ya matumizi ya ardhi.
Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu, Sera na Mawasiliano wa TumeBi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa Mkurugenzi wa Tume
hiyo Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi kazi ya kikosi kazi ya
kukamilisha andiko la Mkakati wa changamoto za mato za matumizi ya Ardhi ikiwa ni pamoja na kuandaa mwongozo na kubadili andiko kwa lugha ya kiingereza ili lipate kusomwa na wafadhili pia wadau wengine.
Afisa Mipango kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald Mwakipesile (wa kwanza kulia) akiwapitisha kikozi kazi katika maeneo mbalimbali ya kukamilisha mkakati wa kutatua changamoto za matumizi ya ardhi nchini.
Afisa Tawala wa Tume ya Taifa ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bi. Nakivona Rajabu akitoa mrejesho wa kikao kilichofanyika na Mh. William Lukuvi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokuwa anakabidhiwa Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi cha
tarehe 14.08.2017 mjini Morogoro.
Wanakikosi kazi wakiwa wanafuatilia mrejesho huo
Wanakikosi kazi wakiwa katika makundi kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja kulibadili andiko la mkakati wa kukabiliana na changamoto za matumizi ya ardhi kwa lugha ya kingeleza ili uweze kuja kusomwa na wafadhiri pamoja na wadau wengine mbalimbali.
Bw. Paulo Tarimo kutoka Wizara ya Kilimo akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Bw. Emmanuel Msofe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, akitoa maoni yake wakati wa mkutano huo.
Bwana Daniel Ouma(kushoto) Afisa Miradi kutoka TNRF akichangia jambo wakati kikosi kazi kikiendelea na kazi.
Bw. Mbaraka Stambuli kiongozi wa Kipengele cha maendeleo ya kisera na kitaasisi katika programu ya kuwezesha umilikishwaji wa Ardhi, akichangia jambo la maboresho wakati wa kubadilisha andiko katika lugha ya kiingereza.
Bwana Herman Nyanda Afisa wanyama pori (TAWA) mwandamizi katika dawati la ushirikishwaji jamii katika uhifadhi wa wanyama pori akichangia hoja wakati shughuli ya kubadilisha andiko katika lugha ya kiingereza inaendela
Kikosi kazi wakiendelea na kazi