Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo Oktoba 24 amemtembelea na kumjulia hali Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya.
Katika safari hiyo, Lowassa alikuwa ameandamana na mke wake, Mama Reginal Lowassa na wameonekana kwenye picha wakiwa na furaha na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Viongozi mbalimbali wa chama hicho wamekuwa wakiendelea kumtembelea na kumjulia hali kiongozi huyo, ambapo hivi karibuni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.
Social Plugin