Mahakama Kuu imesema msanii wa kike katika fani ya uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu anayekabiliwa na kesi ya kuua bila ya kukusudia ana kesi ya kujibu.
Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa fani hiyo, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu, Samu Rumanyika amesema baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi kwa kuita mashahidi wanne amejiridhisha kuwa mshtakiwa ana kesi ya kujibu.
Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lulu ameieleza Mahakama kuwa mshtakiwa atajitetea chini ya kiapo na ameomba muda kwa ajili ya kufanya maandalizi.
Social Plugin