Sehemu ya wananchi wakitoka kwenye semina ya ufugaji bora wa samaki wakati wa Maonesho ya Wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji iliyoandaliwa na Taasisi ya NUEBRAND EC kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Joachim Komba wa Taasisi ya Eden Agri, akitoa elimu ya ufugaji bora wa samaki na faida zake wakati wa semina iliyofanyika wakati wa wiki ya Huduma za Kifedha na Uwekezaji
Wajasiriamali wakiata maelezo kuhusu ufugaji bora wa samaki aina ya kambare waliokuwa wakioneshwa katika banda hilo la Eden Agri
Wananchi wakiwa katika banda la NSSF
Wajasiriamali wakipata maelezo ya jinsi ya kunufaia na Benki ya NMB kuhusu mikopo mbalimbali
Ofisa wa Benki ya Watu wa Zanzibar,Aisha Ali Mohammed akimpatia maelezo mkazi wa Jiji kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo
Maofisa wa Taasisi ya Nuru wakitoa maelezo kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo
Wajasiriamali wakisikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), Neema Fredrick (kushoto) na Godfrey Mshomari kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wajasiriamali wanachama wa mtandao huo. Aliyekaa ni Happiness Mshana.
Ofisa Mkuu wa Elimu kwa Huduma kwa Mlipa Kodi wa TRA, James Mtalika (Kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo wakati wa maonesho hayo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akifafanua jambo kwa wajasiriamali kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo
Meneja Uhusiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), Neema akitoa mafunzo kuhusu ulimaji bora wa kilimo cha mchaichai kinachoendeshwa na mtandao huo
Mabanda ya taasisi zilizoshiriki kwenye maonesho hayo
Maofisa wa Vicoba ambao ni sehemu ya wawezeshaji wa maonesho hayo