MASENETA WA MAREKANI WAKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU DAR ES SALAAM

Rais John Magufuli wa Tanzania, amefanya mazungumzo na ujumbe wa maseneta wa Baraza la Seneti la Marekani.


Taarifa ya Ikulu ya jana Jumatano imesema maseneta hao ni wajumbe wa kamati ya mazingira inayoshughulikia hifadhi ya taifa, wanyamapori na misitu ya Marekani.


Maseneta hao wamekuwepo nchini Tanzania kwa siku tatu lengo likiwa ni kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.


Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk Inmi Patterson.


Taarifa ya Ikulu imewataja maseneta hao kuwa ni James Inhofe, Mike Enzi, David Perdue, Luther Strange, Tim Scott na John Thune.


Baada ya mazungumzo, kwa nyakati tofauti maseneta James Inhofe na Mike Enzi wamemshukuru Rais Magufuli kwa kukutana nao.


Pia, wamemshukuru kwa kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani kuja kuwekeza nchini.


Maseneta hao wamesema Tanzania ina rasilimali nyingi ambazo ni fursa muhimu ya kukuza uchumi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post