Blog yako pendwa iliyo karibu nawe katika kukuhabarisha Leo tarehe 7/10/2017 inasherehekea Mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
MASENGWA BLOG ni Blog yenye makao yake mjini Shinyanga ilianzishwa rasmi Tarehe 7.10.2016.
Mmiliki wa Masengwa Blog Isaac Luhende Masengwa
Blog hii ilianzishwa na Kumilikiwa na Isaac Luhende Masengwa ambaye na yeye pia leo ni siku yake ya kuzaliwa.
Uanzishwaji rasmi wa blog hii ulikuwa tarehe 7.10.2017 saa saba usiku na mpaka sasa inaendeshwa na waandishi wa Habari 4 ambao wamebobea kwenye taaluma hii ya habari.
Uongozi wa MASENGWA BLOG kupitia kwa mkurugenzi wake haiwezi kumsahau mmiliki wa MALUNDE1 BLOG na mwenyekiti wa waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde kwani baada ya Blog hii kuanzishwa alikuwa mtu muhimu katika kushauri, kuelekeza na hata kufanya ili kazi isonge mbele na akaonekana ni mtu anayependa kuona watu wengine pia wakifanikiwa, hawa ni watu wachache sana tulionao katika jamii yetu na ni vema kuwaheshimu kwa sababu ndani ya mioyo yao wamebeba utu.
Sera ya blog hii ni Kutoa habari za uhakika na zisizo fungamana na upande wowote wa kisiasa, kijamii, kiuchumi na kitamaduni ili kutoa habari bila upendeleo na pia hata kwenye soka haifungamani na upande wowote wa timu ili kuendeleza uadilifu wake kila kona.
Masengwa Blog inawaomba wadau wake waendelee kuiamini blog yao kwani na yenyewe kupitia watumishi wake wanazidi kujipanga kuhakikisha inaboresha huduma zake zaidi ya hapa.
MASENGWA BLOG inapenda kutoa shukrani kwa blog rafiki zifuatazo kwa ushirikiano uliopo katikati yake.
MALUNDE1 BLOG
MKALIMANGI BLOG
MPEKUZI BLOG
MILLARDAYOO BLOG
MUUNGWANA BLOG
MTILAH BLOG
KWATA UNIT BLOG
NIJUZE HABARI BLOG
KAMERA YANGU BLOG
UDAKU SPECIAL BLOG
Na blog nyingine nyingi
Social Plugin