Mbunge Ibrahim Abiriga wa manispaa ya Arua
Mahakama moja nchini Uganda imempiga faini ya Shilingi 40,000 za Uganda mbunge mmoja nchini humo kwa makosa ya kukojoa hadharani.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation nchini Kenya Mbunge Ibrahim Abiriga wa manispaa ya Arua siku ya Jumanne aliwasili mbele ya mahakama ya mji wa Kampala na kushtakiwa kwa kukojoa katika ukuta wa jumba la wizara ya fedha.
Alikiri kufanya makosa hayo na akaachiliwa baada ya kulipa faini.
Kwa mujibu wa gazeti hilo Kiongozi wa mashtaka aliiambia mahakama kwamba mbunge huyo alifanya makosa hayo mwezi Septemba 25 mwaka huu katika barabara ya Kyaggwe mjini Kampala.
Upande wa mashtaka ulisema kuwa vitendo vya mbunge huyo vilikuwa kinyume na sheria za baraza la manispaa ya Kampala za 2016.
Kukiri kwake kunajiri baada picha kadhaa za yeye akikojoa kando kando ya barabara kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Chanzo-BBC
Social Plugin