Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI WA CHADEMA ATUPWA RUMANDE KWA LUGHA ZA KICHOCHEZI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam 'limemtupa' rumande Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson.

Kigaila anayetuhumiwa kutoa lugha za kichochezi Oktoba 12 katika mkutano wake na waandishi wa habari, alikutana na kadhia hiyo jana aliporipoti kituoni kituo kikuu cha kanda hiyo.

Mwanasheria wa Kigaila, Frederick Kihwelo akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho leo Jumatatu amesema hatima ya dhamana ya mkurugenzi huyo itaamuliwa kesho Jumanne.

''Amehojiwa kwa masaa 3 kuanzia saa 7 hadi saa 10 na amehojiwa kwa makosa aliyoyafanya katika mkutano wake wa Oktoba 12 na wamekataa kutoa dhamana labda hadi kesho,'' amesema Kihwelo.

''Lakini makosa yake yana dhamana ila wametueleza wanaoweza kuamua ama kupata dhamana au kukosa hawapo ofisini,"

Mwanasheria huyo amesema katika mkutano huo alizungumza mambo mengi ikiwamo kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kutekwa kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.


Mwananchi imezungumza na kaimu kamanda wa kanda hiyo, Benedict Kitalika ambaye amesema upepelezi kwa sehemu kubwa umekamilika.
Chanzo : Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com