Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MVUA YAEZUA MAPAA NA KUANGUSHA NYUMBA ZAIDI YA 10 KATA YA IBADAKULI SHINYANGA

Mvua iliyoambatana na upepo imeezua nyumba zaidi ya kumi katika kata ya Ibadakuli manispaa ya Shinyanga.


Mvua hiyo  iliyoambatana na upepo mkali ilinyesha jana Oktoba 18,2017 jioni na kuezua mapaa na kuangusha baadhi ya nyumba zilijojengwa kwa matofali ya tope.

Diwani viti maalum wa tarafa ya Ibadakuli Mheshimiwa Zuhura Waziri ametembelea wananchi wanalipatwa na majanga hayo na  kuwaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu wakati kamati ya maendeleo ya kata inaendelea kuchukua takwimu sahihi na kuona namna ya kuwapatia msaada wa haraka wa waathirika hao.

Waziri amesema pamoja na kupata majanga hayo ya mvua,amewasihi  wananchi kulima mazao ya chakula pamoja na ya biashara ili kuweza kupata pesa za kujenga nyumba za uhakika na imara.

Amesema kila mtu anajua kuwa kipindi hiki hakuna chakula cha msaada wa moja kwa moja na badala yake kila mwananchi alime na ikitokea kakosa mazao kwa kukosekana kwa mvua za uhakika ndiyo serikali itatoa msaada.
Nyumba ikiwa imeanguka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com