Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA NISHATI SUBIRA MGALU AWAHAKIKISHI WAKAZI WA MBAGALA UMEME WA UHAKIKA


Mhandisi Emanuel Manlabona  akimuonyesha Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu Juu ya uwezo wa kituo  hicho cha kusambaza umeme kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji  Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa
Mhandisi Emanuel Manlabona akimuonyesha Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu Juu ya uwezo wa kituo hicho cha kusambaza umemekulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa 


Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu kulia akisalimiana na mkazi wa Mbagala 
****

Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu amewahakikishia wakazi wa Mbagala umeme wa uhakika kwani wizara  ya nishati kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wa TANESCO  wanafanya jitihada za kutosha kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana  ili kuwezesha matumizi ya viwanda mbalimbali vilivyopo mbagala na matumizi 
ya Nyumbani kwa wakazi wa Mbagala.

“Tumesikia matatizo yenu yanayohusiana na Umeme, 
ila Napenda kuwahakikishiani kuwa Wizaraya Nishati pamoja na  TANESCO kwa ujumla tunafanya kazi, kuhakikisha umeme mbagala unakua  wa Uhakikia, leo hapa nimekuja kutembelea hiki kituo cha usambazaji 
umeme cha mbagala , ambacho kinajengwa na kwa kushirikiana kwa pamoja,  tunapambana kituo hichi kikamilike ndani yam waka huu mpaka kufikia 
Disemba , kituo hiki kiwe kimekamilika".


Hayo aliyazungumza jana katika ziara aliyoifanya 
katika vituo vya kusafirisha umeme, kituo cha Mbagala na Kurasini  lengo kubwa ikiwa ni kuangalia hali halisi ya utendaji wa TANESCO katika 
kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii ya Nishati ya umeme wa uhakika.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com