Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha: KILICHOJIRI KWENYE MAHAFALI YA 20 YA SHULE YA SEKONDARI KANAWA - KISHAPU


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Boniphace Butondo amewaasa wanafunzi wanaotarajia kuhitimu elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kanawa iliyopo  katika kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu kusoma kwa bidii kwa kujikita katika kusoma kwa makundi ili kupeana upeo wa kimasomo ili waweze kufaulu vizuri katika mtihani wao wanaotarajia kuufanya hivi karibuni.



Butondo ametoa nasaha hizo leo Ijumaa Oktoba 20,2017  kwenye mahafali ya  20 ya shule ya Sekondari Kanawa alipohudhuria kama mgeni rasmi.  


Butondo aliwaambia wahitimu hao kuwa usomaji wa kushirikiana ni mzuri na kwamba wakizingatia mbinu hiyo wanaweza kupata ufaulu wa alama za juu.

Amesema usomaji huo wa makundi ni mbinu tosha ambayo itawafanya kupanuana uelewa wa kimasomo ambao utawasaidia kufanya vizuri kwenye mitihani na kisha kujiunga na elimu ya juu.

"Nawaasa wanafunzi mnaohitimu muutumie muda huu mfupi uliosalia kujisomea kwa bidii katika makundi ambayo yatawafanya wote mfaulu," amesema Butondo.

Pia amewataka wanafunzi wanao salia shuleni hapo kuendelea kuonyesha nidhamu kwa walimu wao na kujikita kusoma kwa bidii sanjari na kupenda masomo ya sayansi ambayo yataifanya nchi kuwa na watalaamu wake wenyewe hasa kuelekea Tanzania yenye viwanda.

Nao wazazi waliohudhuria mahafali hayo,  Ester Ishembe amewaasa wanafunzi kuishika sana elimu isiende zake ikiwa huo ndiyo msingi wa maisha yao na wakiichezea watakumbana na ugumu wa maisha uraiani.

Naye mwanafunzi Husna Abdul akisoma risala ya wahitimu hao amesema jumla ya wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne 41, kati yao wasichana  ni 26 na wavulana 15 ambapo walianza Shule mwaka 2014.

Amezitaja baadhi ya changamoto wanazoziacha shuleni hapo kuwa ni ukosefu wa maji safi na salama ,umeme hakuna, vitabu,huduma ya matibabu,pamoja na upungufu wa vitanda 30, ikiwa Shule hiyo ni ya bweni na kutwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Donbosco Nyanda Sylivester amesema mahafali hayo ni 20 ambapo shule ilianza mwaka 1984 na mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 156, wasichana 76 ,wavulana 80.

Amesema Shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye mitihani yake ya kuhitimu kidato cha nne ambapo ni miaka miwili sasa mfululizo haijawahi kupata alama sifuri.

Amesema katika matokeo ya mwaka 2015 ya kidato cha nne wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 57, waliokwenda kidato cha Tano walikuwa 19 huku 38 waliosalia walijiunga na vyuo mbalimbali ikiwemo kwenda Jeshi na hakuna aliyepata sifuri.

Amesema Mwaka 2016 ,waliofanya mtihani wa kuhitimu walikuwa 46, wanafunzi 29 walijiunga na kidato cha tano ,huku 17 waliosalia nao hakuna aliyepata alama sifuri.

Aidha Katika utatuzi wa changamoto hizo mgeni Rasmi Boniphace Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana wilayani Kishapu ,aliahidi kuzibeba na kuzitafutia ufumbuzi likiwemo suala la kuvuta maji shuleni hapo.

Hata hivyo kwa baadhi ya changamoto alizitatua hapo hapo kwa kushirikiana na viongozi wa CCM wilayani humo, na baadhi ya madiwani alioambatana nao kwa kulimazia suala la uhaba wa vitanda hivyo 30 pamoja na kupatikana fedha za kufunga nyaya kwa ajili ya kuvuta umeme shuleni hapo ,mbapo zilipatikana shilingi Milioni 3 kutoka kwa mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akiwakilishwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu Helena Chacha.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO
Mgeni rasmi,Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu ,mheshimiwa Boniface Butondo akizungumzakatika mahafali  ya 20 ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kanawa,-Picha zote na Marco Maduhu -  Malunde1 blog
Mheshimiwa Butondo akizungumza
Wahitimu wakimsikiliza mgeni rasmi
Mheshimiwa Butondo akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii
Mzazi Ester Ishembe akitoa Nasaha kwa wanafunzi wanao tarajia kuhitimu kidato cha Nne na wanao salia Katika Shule ya Sekondari Kanawa wilayani Kishapu.
Mwanafunzi Husna Abdul (kushoto) akisoma risala ya wahitimu kwa kushirikiana na mwenzake Patrick Petro ,kuwa walianza Masomo Mwaka 2014, na wanahitimu wanafunzi 41 ,wasichana 26, wavulana 15.
Wazazi wakiwa kwenye mahafali
Wazazi wakiwa katika eneo la tukio
Wahitimu kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kanawa iliyopo wilayani Kishapu ,wakiwa kwenye mahafali yao 
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kanawa Donbosco Nyanda Sylvester akisoma taarifa ya Shule hiyo na kusema ilianza mwaka 1984 na imekuwa ikifanya vizuri kitalaamu, na miaka miwili sasa hakuna mwanafunzi aliyepata alama sifuri.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo akisikiliza somo la Biology kutoka kwa mwanafunzi Rehema Rajabu wa kidato cha tatu katika shule hiyo ya Kanawa
Mwanafunzi Irene Daudi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Kanawa wilayani Kishapu akimuonyesha mgeni rasmi namna ya kupima joto la chumvi, katika maabara ya Chemistry shuleni hapo
Mwanafunzi akionesha kwa vitendo jinsi alivyobobea katika masuala ya kwenye maabara
Picha ya Pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne na mgeni rasmi
Mgeni rasmi akitoa cheti kwa mmoja wa wanafunzi wa kidato cha nne wanaohitimu masomo yao mwaka huu
Mgeni rasmi akitoa cheti kwa mwanafunzi.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com