Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : MWILI WA MWANDISHI WA HABARI ANCETH NYAHORE WAZIKWA JIJINI MWANZA

Mwili wa mwandishi wa Habari Anceth Nyahore aliyefariki dunia Oktoba 21,2017 umezikwa leo Oktoba 25,2017 katika makaburi ya Nyasaka jijini Mwanza.


Nyahore alifariki dunia wakati  akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Sekouture jijini Mwanza.

Nyahore alikuwa akiandikia gazeti ya Nipashe,The Guardian na Zanzibarleo katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.

Nyahore pia aliwahi kufanya kazi na ITV na Radio One.

Nyahore alizaliwa Mei 10,1962 mkoani Mara,ameacha mjane,watoto watatu na wajukuu watatu.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Anceth Nyahore. Amina.

 Anceth Nyahore enzi za uhai wake
Ndugu za marehemu wakiaga mwili wa marehemu Anceth Nyahore (katikati ni mama mzazi wa Anceth Nyahore)

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu likiwa katika makaburi ya Nyasaka - Mwanza

Jeneza likiingizwa kaburini

Mazishi yanaendelea

Wakazi wa Nyasaka pamoja na waandishi wa habari mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakiwa katika kaburi la marehemu Anceth Nyahore

Mama mzazi wa Anceth Nyahore akiweka shada la maua katika kaburi la mwanae
Kiongozi wa dini akiweka shada la maua
Wanahabari baada ya kuweka shada la maua
Waandishi wa habari mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakiweka shada la maua
Kaka mkubwa wa Anceth Nyahore na mkewe wakiweka shada la maua

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com