Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : SHULE YA KOM SEKONDARI YAUNGA MKONO KAMPENI YA KUPANDA MITI SHINYANGA

Shule ya Sekondari KOM (Kom Sekondari) iliyopo katika eneo la Butengwa mjini Shinyanga,imeunga mkono kampeni ya upandaji miti yenye kauli mbiu ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ kwa kupanda miti 482 katika barabara ya Shinyanga Mjini kuelekea Old Shinyanga.

Zoezi la upandaji miti limefanyika leo Jumamosi Oktoba 21,2017 likiongozwa na Mkuu wa shule ya Kom Sekondari Mwita Warioba,walimu na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mkuu huyo wa shule,Mwita Warioba alisema pamoja na shule hiyo kuwa na utaratibu wa kupanda miti lakini wameamua kuunga mkono jitihada za Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuhamasisha jamii kupanda miti ili kukabiliana na hali ya jangwa.

“Kom Sekondari haiko tayari kuona Shinyanga inageuka jangwa hivyo tunaunga mkono kampeni ya upandaji miti,tunapanda miti 482 katika eneo la urefu wa kilomita 2.4 katika barabara hii iliyopo karibu na shule yetu,tutaitunza na kuhakikisha inakua”,alieleza Warioba.

Alisema shule hiyo imekuwa mstari wa mbele katika suala la upandaji miti mpaka sasa shule inazungukwa na takribani miti 6000.
 
ANGALIA PICHA WAKATI ZOEZI LA UPANDAJI MITI LIKIFANYIKA
Mkuu wa shule ya Kom Sekondari Mwita Warioba akichimba shimo kwa ajili ya kupanda mti katika barabara ya kuu ya kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Old Shinyanga iliyopo karibu na shule hiyo leo Jumamosi Oktoba 21,2017-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa shule ya Kom Sekondari Mwita Warioba akiendelea kuchimba shimo kwa ajili ya kupanda mti,kushoto ni wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo
Wanafunzi wakichimba mashimo kwa ajili ya kupanda miti
Wanafunzi wakiendelea kuchimba mashimo
Zoezi la uchimbaji miti likiendelea
Mwalimu Neema Daniel akishiriki zoezi la uchimbaji mashimo
Mkuu wa shule ya Kom Sekondari Mwita Warioba akipanda mti
Mkuu wa shule ya Kom Sekondari Mwita Warioba akiweka udongo kwenye mti alioupanda wakati wa zoezi la upandaji miti katika barabara ya Shinyanga Mjini - Old Shinyanga.
Wanafunzi wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mwalimu wao wakati wa zoezi la upandaji miti
Muonekano wa miti iliyopo katika lango la kuingia katika shule ya sekondari Kom.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com