Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika eneo la Bugayambele kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga leo Alhamis Oktoba 26,2017 wametembelea kituo cha watoto wenye ualbino cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa na wanafunzi hao waliokuwa wameongozana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Paul Kiondo ni pamoja na nguo,viatu,sabuni,mchele,mabegi ya shule,madaftari,kalamu,pipi,biskuti,sukari,miswaki na dawa ya meno.
Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Little Treasures Paul Kiondo amesema shule hiyo imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kwa wanafunzi wao kutembelea kituo cha Buhangija kwa ajili ya watoto kubadilishana mawazo na kuwapatia zawadi mbalimbali watoto waliopo katika kituo hicho.
“Little Treasures imekuwa karibu na kituo hiki,na kila mwaka tumekuwa tukiwaleta wanafunzi wetu hapa kuwasalimia watoto wenzao,lakini pia tumekuwa tukiwahamasisha wanafunzi wetu kuwaomba wazazi wao wawape chochote ili wawapelekee watoto wenzao waliopo katika kituo cha Buhangija”,alieleza Kiondo.
Wanafunzi 81 kuanzia darasa la awali hadi la sita wamefika katika kituo cha Buhangija kuwawakilisha wanafunzi wengine zaidi ya 600 wanaosoma katika shule hiyo.
Shule ya msingi Little Treasures ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika mitihani mbalimbali ambapo katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2017 katika kundi la shule zenye watahaniwa pungufu ya 40 imeshika nafasi 1 kati ya 14 katika wilaya ya Shinyanga nafasi ya kimkoa 7 kati ya shule 231 na ya 64 kitaifa kati ya 6839. Angalia Matokeo <<HAPA>>
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WANAFUNZI WA SHULE YA LITTLE TREASURES WALIPOTEMBELEA KITUO CHA BUHANGIJA
Mlezi wa wanafunzi waliopo katika kituo cha Buhangija Flora Kankutebe akiwakaribisha wanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures walipotembelea kituo hicho leo Oktoba 26,2017.-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Wanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures wakijitambulisha kwa kunyoosha mikono
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akizungumza wakati wa ziara ya wanafunzi wa shule hiyo walipotembelea kituo cha Buhangija.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiwa na mwalimu wao wakifurahia jambo kwa kupiga makofi katika kituo cha Buhangija
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiwa katika kituo cha Buhangija
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiwa katika kituo cha Buhangija
Kulia ni Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akitambulisha wafanyakazi wa shule ya msingi Little Treasures
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akiongea na watoto waliopo katika kituo cha Buhangija kabla ya zoezi la ugawaji zawadi
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo akielezea kuhusu zawadi zilizotolewa na wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Little Treasures.Pichani ni zawadi hizo ambazo ni nguo,sabuni,mabegi ya shule,madaftari,kalamu,mchele,sukari
Wafanyakazi kutoka shule ya Little Treasures wakipanga vizuri zawadi hizo kabla ya zoezi la ugawaji kuanza
Wanafunzi wa shule ya Little Treasures(kulia),wakijiandaa kugawa zawadi kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Wanafunzi wa shule ya Little Treasures wakiwa wamebeba zawadi kabla ya kuanza kukabidhi kwa wanafunzi/watoto wanaolelewa katika katika kituo cha Buhangija
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures akigawa zawadi ya biskuti kwa mwanafunzi anayesoma katika shule ya msingi Buhangija anayelelewa katika kituo cha Buhangija
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures akigawa zawadi ya begi la shule
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Little Treasures akigawa zawadi ya sabuni
Zoezi la utoaji zawadi linaendelea
Zoezi la kugawa zawadi linaendelea
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Little Treasures Paul Kiondo na Msimamizi wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya wakipanda mti wa kumbukumbu katika kituo cha Buhangija
Mwanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures akimwagia maji mti huo wa kumbukumbu
Wafanyakazi,Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures na wanafunzi/watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakiwa katika picha ya pamoja
Picha ya kumbukumbu
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakijiandaa kupanda kwenye magari ili warudi shule kuendelea na masomo yao
Moja ya magari ya shule ya msingi Little Treasures ikiondoka katika kituo cha Buhangija.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin