Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo hii amemteua Profesa Florenss Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania badala ya Profesa Benno Ndulu ambaye ameombwa kukabidhi ofisi haraka.
Rais Magufuli amteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania. Amtaka Gavana wa sasa Beno Ndulu kuanza utaratibu wa kukabidhi ofisi haraka.
Rais Magufuli alifanya uteuzi huo wakati wakati wa kutunuku vyeti vya pongezi maalum wajumbe wote waliohusika kuchunguza kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Luoga alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA).
HII HAPA TAARIFA KUTOKA IKULU
Social Plugin