Afisa Mradi kutoka UNA Tanzania, Saddam Khalfan akielezea kuhusu mradi wa Kuwajengea uwezo vijana kushiriki katika michakato ya maamuzi na utekelezaji wa sera ya maendeleo ya vijana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwenye Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika lililofanyika katika Viwanja vya Furahisha, Jijini Mwanza. Mradi huo unatekelezwa na asasi za vijana kumi na saba Tanzania bara na Visiwani chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society. Kushoto ni Kaimu Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, William Mnyippembe.
Mgeni rasmi Kaimu Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, William Mnyippembe akifungua Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika kwa kutoa ujumbe kwa vijana kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kujiendeleza kielimu na kukuza kipato.
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Mwanza, Gilbert Otieno akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika lililowakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya za Nyamagana na Ilemela lililolenga kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo, michakato ya maamuzi na kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za chini hadi juu pamoja na kuongeza uelewa wao juu ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngaza wakiimba shairi la kuhamasisha vijana kushiriki katika michakato ya maamuzi na kutobaki nyuma katika kujitafutia taarifa za maendeleo.
Mkurugenzi wa YEV Mwanza, Jonathan Kassibu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika na kazi za taasisi yake ya kuunda majukwaa ya vijana na kuwajengea uwezo vijana katika kata nne za Manispaa ya Nyamagana, jijini Mwanza chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwanza wakiimba wimbo wa AMKA KIJANA ambao ulilenga kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa na kutokubweteka.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika shindano la uchoraji wa picha za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakionyesha picha hizo kwa washiriki na majaji wakati wa Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika lililofanyika jijini Mwanza.
Wanafunzi wakiwashangilia washiriki wa shindano la uchoraji wa Picha ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.
Wanafunzi wakiigiza kuhusu Tabia za Vijana na mienendo yao wakati wa Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika liliondaliwa na UNA Tanzania, YEV Mwanza kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika liliondaliwa na UNA Tanzania, YEV Mwanza kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society.
Msanii wa miondoko ya 'HipHop' nchini Tanzania, Kala Jeremiah akitumbuiza wimbo wake mpya wa KIJANA ambao unalenga kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo na kushiriki katika michakato ya maamuzi na kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya chini hadi juu katika Tamasha la Kijana Paza Sauti, Wajibika liliondaliwa na UNA Tanzania, YEV Mwanza kupitia ufadhili wa The Foundation For Civil Society. Tamasha hili limefanyika katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza.
Social Plugin