Mwandishi wa habari Mwandamizi nchini Tanzania Anceth Andrew Nyahore amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Sekouture jijini Mwanza.
Nyahore amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili Oktoba 22,2017.
Nyahore alikuwa akiandikia gazeti ya Nipashe,The Guardian na Zanzibarleo.
Nyahore pia aliwahi kufanya kazi na ITV na Radio One.
Nyahore pia aliwahi kufanya kazi na ITV na Radio One.
Taarifa za kifo cha Nyahore zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Simiyu Frank Kasamwa na kwamba taarifa zaidi kuhusu msiba zitatolewa.
Kabla ya kuhamia mkoani Simiyu,Nyahore alikuwa anafanya shughuli za uandishi wa habari mkoani Shinyanga.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Anceth Nyahore.Amina.
Nyahore enzi za uhai wake akitekeleza majukumu yake
Social Plugin