Mwezeshaji wa semina Joe Nakajumo akifundisha katika mafunzo hayo leo Mkoani Morogoro
Kushoto ni Noria Damian ,katikati Editha Carlo pamoja Happines Mtweve wakifuatilia mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini wakifatilia mafunzo hayo kwa ukaribu
Amon Mtega kutoka Ruvuma Press club akichangia mada katika mafunzo hayo ,kulia ni Queen Isack kutoka Kilimanjaro Press Club
Kushoto ni mwakilishi kutoka Arusha Press club Pamela Mollel,katikati ni Adam Juma kutoka Mtwara Press Club wakifatilia mafunzo
Mwandishi wa habari Laudence Simkonda kutoka Mbeya kulia Oscar Simon kutoka Rukwa wakifuatilia mafunzo hayo
****
Waandishi nchini wametakiwa kuongeza muamko katika kuandika na kutangaza habari za vijijini kwa kuwa asilimia 75ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini ambako
wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali.
Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Morogoro na mwenzeshaji Joe Nakajumo katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini iliyowakutanisha wanahabari kutoka mikoa mbalimbali iliyoratibiwa na umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC)
Nakajumo alisema kuwa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kuwa karibu na jamii ya vijijini kwa kutambua shughuli zao wanazozifanya na kuzifatilia kwa kuona
mafanikio yao pamoja na kuibua kero zinazowakabili
“Asilimia 75 ya wananchi wanaishi vijijini wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za kilimo,ufugaji ,uvuvi,ujasiriamali hivyo ni muhimu sana kuwapa kipaumbele wananchi hawa”,alisema Nakajumo.
Aidha alisema moja ya majukumu ya msingi ya mwandishi wa habari ni kusaidia na kushiriki katika ujenzi wa taifa hivyo anapaswa kuudhihirishia umma kwa watu wote nchini wanapaswa kupata habari.
Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo Adam Juma alisema kuwa mafunzo haya yatasaidia kuibua changamoto vijijini ambako panaoneka kusaulika kwa huduma mbalimbali za kijamii.
Pia aliwaomba waandaji wa semina hii UTPC kuendeleza mafunzo haya kwa waandishi wa habari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya
taaluma hiyo
UTPC imeendelea kutoa mafunzo mbalimbali
kwa waandishi wa habari lengo ikiwa kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya taaluma ya uandishi wa habari.
Na Pamela Mollel,Morogoro