Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

YANGA WAITWANGA STAND UNITED 4 - 0

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara misimu mitatu mfululizo,Yanga leo wameibuka na ushindi mnono wa magoli manne kwa bila dhidi ya Stand United katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.

Magoli hayo yamefungwa na Ajib amefunga magoli mawili,Buswita goli moja na la nne limefungwa na Obrey Chirwa.

Hii ni kama kujibu salamu kwa watani wao wa jadi Simba ambao jana waliibuka na Ushindi wa goli nne kwa bila dhidi ya timu ya Njombe mji.

Kwa matokeo hayo sasa Yanga wanakaa nafasi ya pili wakiwa na point 15 sawa na Simba ,tofauiti ni magoli ya kufunga na Kufungwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com