Konokono ni moja kati ya viumbe wenye mwendo wa taratibu sana duniani, tofauti na hilo zipo jamii ambazo wanakula nyama ya Konokono na jamii nyingine hazitaki hata kuamini kwamba kuna watu kwenye dunia hii wanakula Konokono.
Hata hivyo, watafiti hasa wa afya na tiba ya binadamu wamechunguza na kugundua kuwa Konokono akipikwa na kuliwa kama chakula cha kawaida ana virutubisho ambavyo ni faida kubwa kwa binadamu kwa kuponya magonjwa mbalimbali.
Kati ya virutubisho vinavyopatikana katika nyama ya Konokono ni vitamin na protini nyingi, asidi za amino na vingine vingi.
1. Huongeza ufanisi kwenye Ubongo
Konokono anasifika kwa kuwa na mafuta yenye kiambata cha Omega 3 ambacho husaidia katika maendeleo ya ubongo na kumbukumbu hususani kwa watoto kwasababu husaidia uboreshwaji wa seli za mwili.
2. Chanzo kikubwa cha Vitamin
Kiumbe hiki kina utajiri mkubwa wa vitamini A, E, B1, B3, B6 na B12. Vitamini A hufanya kazi ya kuboresha afya ya macho lakini pia Omega 3 inayopatikana kwenye konokono huwa na msaada wa kiafya kwa wamama wajawazito.
3. Huboresha ukuaji wa mifupa
Konokono pia anatajwa kuwa na wingi wa madini ya magnesium ambayo huratibu mifumo yote ya ukuaji na uboreshwaji wa mifupa mwilini.
4. Huboresha afya ya moyo
Kiumbe huyu pia anaripotiwa kuwa na Potasium nyingi na sodium kidogo jambo ambalo linaleta uwiano mzuri wa madini ambayo yanaweza kuweka sawa viwango vya msukumo wa damu ikiwa ni pamoja na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kiharusi na figo.
5. Hupambana na Saratani
Pia moja ya vitu ambavyo nyama ya konokono hufanya mwilini ni kupambana na saratani. Kinga hii inapatikana katika uteute wa konokono ambao ndio huongeza kinga ya mwili kupambana na saratani za aina zote.
6. Huboresha uzalishwaji wa seli
Konokono pia anasifika kwa kuwa na madini ya chuma ambayo husaidia sana katika kuzalisha na kuboresha seli za mwili, zoezi ambalo linafanyika kila siku.