Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishindana kucheza muziki na watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija wakati wa hafla ya kula chakula cha pamoja kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited-Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameshiriki katika hafla fupi kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija mjini Shinyanga kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited inayomilikiwa na Crissant Mssipi.
Kabla ya kula cha pamoja na watoto hao,mkuu huyo wa wilaya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ulinzi walifanya usafi wa mazingira ikiwemo kupulizia dawa ya kuua wadudu kama vile kunguni katika mabweni yanayotumiwa na watoto hao.
Hafla fupi ya chakula cha pamoja iliyohudhuriwa pia na Afisa Mthibiti ubora wa Shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga,imenogeshwa kwa burudani ya muziki ambapo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro aliamua kucheza muziki na watoto hao hali iliyoongeza furaha zaidi kwa watoto hao.
Akizungumza katika kituo hicho,Matiro ameitaka jamii kuondokana na dhana ya kuwabagua na kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kukata viungo na kuwaua akibainisha kuwa watoto wenye ualbino binadamu kama wengine na kinacho watofautisha ni rangi tu ya ngozi yao.
Amesema jamii ikibadilika watoto hao wataishi kwa amani na furaha kwa kujiona hawana tofauti na binadamu wengine .
"Naomba jamii iondokane na matukio ya kuwanyanyasa watoto hawa ili nao waishi kwa amani na upendo ," amesema Matiro
Aidha alisema hivi karibuni serikali iliamua kuwarudisha majumbani baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi katika kituo hicho wakiwemo waliohitimu elimu yao ya msingi katika Shule ya Buhaghija hivyo akaitaka jamii kuhakikisha inawalinda na wanaishi kwa amani bila ya kubughudhiwa.
Naye msemaji wa Kampuni hiyo ya Ulinzi Twaha Makani, amesema mara baada ya siku chache kukitembelea kituo hicho waliguswa na vitu vingi vinavyohusu maisha ya watoto hao na hivyo kuamua kufanya shughuli za usafi wa mazingira, kupulizia dawa ya kuua kunguni pamoja na kula nao chakula cha pamoja.
Kwa upande wake mmoja wa walezi wa kituo hicho Bright Mduma mbali na kuishukuru kampuni hiyo ya ulinzi kwa kufanya usafi,kuua wadudu na kuandaa chakula,amesema kituo hicho kina jumla ya watoto 228, watoto wenye ualbino 144, wasiosikia 60 na wasioona 24.
Mwandishi wa Malunde1 blog,Marco Maduhu alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha za matukio yaliyojiri
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza katika hafla fupi ya kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga ambapo aliwahakikishia ulinzi pamoja na kuboreshewa makazi yao.-Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Msemaji wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza na watoto hao ambapo alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana nao kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaendelea kuwakabili.
Msemaji wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza katika kituo cha Buhangija
Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga, akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija ambapo aliwataka wadau wajitokeze kuwasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili pamoja na kushiriki kula nao chakula cha pamoja na siyo kusubiri hadi siku za sikukuu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD wakipulizia dawa ya kuua kunguni katika mabweni ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Zoezi la kupulizia dawa ya kuua wadudu likiendelea
Sehemu ya Mashuka yakiwa yameanikwa baada ya kufuliwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD wakipulizia dawa ya kuua kunguni katika mabweni ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija
Zoezi la kupulizia dawa ya kuua wadudu likiendelea
Sehemu ya Mashuka yakiwa yameanikwa baada ya kufuliwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akipika chakula kwa ajili ya watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga
Watoto wenye ualbino wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD
Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD
Watoto wakiendelea kula chakula
Baadhi ya walinzi wa kampuni hiyo nao wakishiriki kula chakula cha pamoja na watoto hao
Zoezi la kula chakula likiendelea
Watoto wakila chakula
Mtoto akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) uwezo wake wa kucheza muziki
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) akicheza muziki wimbo wa Diamond Platnumz zilipendwa na watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija
Mimi ni nomaaaa!! subiri nikuoneshe kazi mkuu.......
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akifurahia show ya mtoto.....
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza na watoto hao
Kushoto ni Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga akicheza muziki
Watoto wakicheza mziki wa Kamatia chini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza Kwaito na watoto hao
Watoto wakicheza muziki na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Watoto wakisakata rhumba
Watoto wakiendelea kucheza
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Social Plugin