Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA UBA TANZANIA YATOA MSAADA WA VITABU 800 SHULE YA BARBRO JOHANSON


Mkurugenzi mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote baadhi ya vitabu kwaajili ya wanafunzi kujisomea na kuongeza maarifa kupitia vitabu hivyo ambavyo vimetolewa kwa msaada na benki ya UBA Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa benki ya UBA Tanzania akiongea na mkuu wa shule ya sekondari ya Barbro Johanson pamoja na wafanyakazi wa benki ya UBA na shule hio mara baada ya kukaribishwa ofisini kwa mkuu wa shule hiyo Bi Halima Kamote  jana
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote akiangalia moja ya vitabu mia nane vilivyotolewa na benki ya Uba katika kuendeleza juhudi zao za kurudisha faida kwa jamii. Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA Tanzania Bw Peter Makau.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Barbro Johanson, Bi Halima Kamote akiongea na wafanyakazi wa benki pamoja na shule hio katika ofisi yake mara baada ya kupokea ugeni kutoka benki ya UBA Tanzania ambao walifika shule hapo kwaajili ya kukabidhi msaada wa vitabu takribani mia nane vya kujisomea msaada ambao umekabidhiwa kwa mkuu wa shule hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau akimkabidhi mmoja wa wanafunzi wa shule ya Barbro Johanson moja ya vitabu vilivyotolewa na benki hiyo kama mchango wake kwa jamii. Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

***
Katika kuendeleza kwake kuhakikisha wanafunzi wanaendelea kusoma na kupata vifaa mbalimbali vya kukuza taaluma zao, jana benki ya Uba Tanzania walitoa msaada wa Vitabu takribani 800 vya kiada ambavyo vitasaidia kuongeza hali ya usomaji kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Msaada huo wa vitabu zaidi ya mia nane ulitolewa mapema jana shule hapo na kukabidhiwa mkuu wa shule hiyo Bi, Halima Kamote huku Mkuu wa shule hio akiishukuru benki hio kwa kujitoa kwake katika kusaidia kuongeza vitabu vya kujisomea kwa wanafunzi wa shule huku akisema amefurahishwa na benki hiyo kwa msaada huo na kuwakaribisha tena pale ambapo wataguswa kuchangia zaidi na zaidi.

Naye mmoja wa wanafunzi aliyepokea kitabu kwa niaba ya wanafunzi wenzake ameishukuru pia benki ya UBA kwa msaada huo wa vitabu kwa maana itaongeza hali ya kujisomea na kuongeza ujuzi katika mawasiliano ambapo somo la Ujuzi wa Mawasiliano limekuwa moja ya somo katika Shule hiyo huku likiwa halipo kwenye mitaala ya kufundishwa katika shule za sekondari hapa nchini.

Benki ya Uba imekuwa moja ya benki ya kibiashara hapa nchini katika Kuchangia maswala mbalimbali ya kijamii huku ikirudisha faida yake kwa jamii iliyowazunguka.
Imeandikwa na Josephat Lukaza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com