Taarifa iliyotolewa leo Alhamis Novemba 23,2017 na Ikulu imesema Dkt. Slaa ataapishwa baada ya taratibu zote kukamilika.
Dkt. Slaa ambaye kwa sasa anaishi Canada alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa Ukawa.
Dkt. Slaa alisema chama chake hakikutekeleza makubaliano waliyoafikiana ya kuwapokea baadhi ya makada wa CCM akiwemo Lowassa.
Kiongozi huyo alisema anasimamia ukweli na dhamira yake imemfanya ashindwe kumuunga mkono mgombea ambaye amekuwa akimtuhumu kwenye majukwaa.
Alisisitiza kuwa asingehamia chama chochote cha siasa bali angeendelea kutoa mchango wake kwa umma wa Watanzania nje ya vyama vya siasa.
Social Plugin