Katika dakika chache zilizopita , spika wa bung la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu.
Kumekuwa na shangwe miongoni mwa wabunge kufuatia tangazo hilo.
Harakati za kumuondoa madarakani rais huyo kupitia bunge kumesitishwa.habari za kujiuzulu kwake zilitolewa wakati wabunge walipokuwa wakijiandaa kuanza harakati za kumngoa madarakani kupitia bungeni.katika barabara za Harare kulikuwa na sherehe huku magari mengi yakipiga honi.
Mwaka 1980, Bw Mugabe alishinda uchaguzi na kuwa waziri mkuu.
Mwaka 1982 aliushutumu upinzani kwa kujaribu kupindua serikali.
Maelfu ya watu waliuawa alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui zake.
Mwaka 1987,alibadilisha katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake.
Uchumi ulidorora baada ya mwaka 2000
Wakati Mugabe aliagiza kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi.
Mfumuko wa bei ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi kudororeka.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.
Japo kulikuwa na ghasia dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi.
Ndoa yake na Grace Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza.
Wengi walikasirishwa na Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.
Jeshi limeonesha kumtaka Emmerson Mnangagwa aliyefutwa kazi kama makamu wa Rais na Mugabe mwezi Novemba.
Social Plugin