Nahodha
na beki mkongwe wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, yupo kwenye
mazungumzo ya mwisho na klabu yake hiyo ya kuongeza mkataba mwingine wa
miaka miwili.
Beki huyo alijiunga na Yanga kwenye msimu wa 2006/07 akitokea Zanzibar alipokuwa anacheza soka kabla ya kutua Jangwani.
Cannavaro
tangu ajiunge na Yanga hajaihama timu hiyo hadi hivi sasa huku
akifanikiwa kubeba makombe matatu ya Ligi Kuu Bara, Ngao ya Jamii mbili
na Kombe la FA mara moja na Kombe la Chalenji akinyanyua mara moja.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Cannavaro alisema wakati wowote anatarajiwa
kusaini mkataba mara baada ya kufikia makubaliano mazuri na viongozi wa
timu hiyo.
Cannavaro
alisema anaamini miaka miwili hiyo ndiyo ya mwisho kwake kuendelea
kucheza soka ambayo mara baada ya kumalizika, basi atatangaza rasmi
kustaafu.
Aliongeza kuwa, mara baada ya kustaafu soka, haraka ataanza kozi ya ukocha ili baadaye katika maisha yake awe kocha.
“Mimi
nina miaka yangu miwili ya kucheza soka pekee na badala yake
nitawaachia wachezaji wengine vijana ili wapate nafasi ya kuonekana
katika soka.
“Hivyo,
hivi sasa nipo mimi nipo kwenye mazungumzo na mabosi wangu wa Yanga kwa
ajili ya kuongeza miaka miwili ya mwisho,” alisema Cannavaro.