Sakata la kumvua madaraka Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza James Bwire, limechukua sura mpya baada ya kikao cha baraza la madiwani kuvunjika, kutokana na madai kuwa baraza hilo halitaendesha vikao vyake hadi muafaka wa sakata hilo utakapopatikana.
Hiki ni kikao cha pili tangu sakata hilo lilipoanza kufukuta ndani ya Halmashauri hiyo, ambapo makundi mawili ya madiwani yanasigana, huku moja likisema kuwa linamhitaji Meya huyo na jingine likisema kamwe halimhitaji, kwa mujibu wa kikao cha kwanza cha baraza la madiwani.
Kutokana na misimamo hiyo ya Madiwani, kikao hiki cha pili kilichodumu kwa zaidi ya saa tatu kilivunjika bila kuwepo mjadala wowote, huku madiwani wakiburudishwa na wimbo wa maadili ya kazi ndani ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Muda mfupi baadaye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Kiomon Kibamba akawasili ndani ya ukumbi na kisha kutamka neon moja kwa madiwani hao, waliokuwa wamejiandaa kwa ajili ya mjadala.
Kisha madiwani Madiwani hao wakaanza kutoka ndani ya ukumbi, huku wakiwa wamefunika midomo kwa viganja, ikiwa ni ishara ya kutotaka kuzungumzia sakata hilo, ingawa Madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walitoa msimamo wao.
Sakata la kuvuliwa madaraka la Mstahiki meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, bado linaendelea kuwa kitendawili Jijini hapa, ambapo kwa mujibu wa Meya huyo sababu zinazolenga kutaka kumvua madaraka zinatokana na uwajibikaji wake