Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo alimtembelea na kumjulia hali Mzee Abdulrazack Mussa Simai 'Kwacha' ambaye amelazwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI).
Mzee Abdulrazack Mussa Simai 'Kwacha' ni Mzee wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia alishawahi shika nafasi mbali mbali za Uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Social Plugin