Makubwa Haya!! Ndivyo unaweza kusema...Kutoka Arusha tunaambiwa kuwa kijana aliyejulikana kwa jina la Musa Shakifu amekamatwa na jeshi la polisi baada ya kuvamia shule ya Msingi Oltroto iliyopo Arumeru na kutaka kuwabaka kwa mara moja walimu pamoja na wanafunzi.
Hata hivyo kijana huyo hakufanikiwa kwenye jaribu hilo la kutaka kubaka walimu na wanafunzi na tayari Jeshi la Polisi limekamata ambapo Kamanda wa Polisi Charles Mkumbo amesema wanaendelea kumuhoji.
Mwalimu wa zamu kwenye shule hiyo amekiri kuvamiwa na kijana Musa ambaye alionekana kutumia nguvu za kupitiliza kutaka kuwabaka kwa mkupuo walimu pamoja na wanafunzi.
Social Plugin